Inter Rasmi Kumtia Mikononi Lukaku

Klabu ya Inter Milan imethibitisha kuwa wamefanya mkutano rasmi na klabu ya Manchester United kumzungumzia nyota wa klabu hiyo Romelo Lukaku.

Inter walikuwa wakihusishwa na nyota huyu mapema kabla na wakaamua kuwatuma maafisa wake Uingereza kwa ajili ya kumfikia staa huyu na kujaribu kumpeleka pale Italia.

Lukaku alisaini mkataba na klabu ya Manchester United akitokea Everton kwa dau la paundi milioni 75 mwaka 2017.

Mkurugenzi wa michezo wa Piero Ausilio, amesema kwa walikuwa na mkutano na Manchester United kumhusu Lukaku. Hajaweka wazi undani wa mazungumzo hayo.

Lukaku alikuwa akiweka bayana mapenzi yake ya kwenda kucheza soka Italia tangu awali alipokuwa anahusishwa na klabu hiyo ya Inter Milan.

Staa huyu anaweza kutemana Ole Gunar msimu unaokuja akiwa amewachapia magoli 12 Manchester United msimu uliopita. Msimu ujao anaweza kuwa anatia kazi na miamba wa Serie A.

2 Komentara

    Habari njema.

    Jibu

    Lukaku hana makali tena uwezo wake ushaisha sijui kama hatafanya vizuri hapo inter

    Jibu

Acha ujumbe