Inter Milan wamepata hasara ya €102.4m mwaka ulioishia Juni 2020, na mapato yakipungua kwa €45m.”Tuliweka misingi imara ambayo kadri mda unavyozidi kwenda itaturuhusu kufanikiwa tena.”

Klabu hiyo ilitoa takwimu zake wakati wa mkutano wa wabia, ambao ulifanyika kupitia teknolojia ya video.

Kimsingi, uchumi uiliathiriwa vibaya na janga la corona na kufungwa kwa viwanja, na kusababisha kutokuwa na mapato ambayo hupatikana kutokana na mauzo ya tiketi.

Inter pia ilikuwa moja ya vilabu vya Serie A vilivyopaswa kulipia tiketi za msimu za wateja.

Mapato yalipungua kwa €45m ikilinganishwa na mwaka jana, imejumuishwa kwa € 372.4m, na klabu imepata hasara ya €102.4m msimu uliopita.

Rais Steven Zhang amesema Inter imepitia mtikisiko mkubwa wa kiuchumi, lakini kupitia mtikisiko huo wameweza kuweka mipango mbadala ya maendeleo ya klabu, na wanaamini itarejesha matunda mema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Michezo, Giuseppe Marotta pia alizungumza kwenye mkutano huo na kuhakikishia Inter walikuwa kwenye njia sahihi katika kurejea kwenye mstari.

“Tuliweka misingi imara ambayo Tuliweka misingi imara ambayo kadri mda unavyozidi kwenda itaturuhusu kufanikiwa tena. Lengo letu linabaki kuboresha matokeo kila wakati, msimu baada ya msimu.”


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa