Sio mbaya kubadilisha mazingira au mbinu pale ambapo unayoitumia haikupi matokeo unayoyatarajia. Isco Alcaron anahitaji kujaribu kucheza kwenye ligi nyingine.

Kiungo huyo amekuwa na wakati mgumu ndani ya La Liga na Real Madrid, kwa msimu huu pekee – amecheza michezo 3 tu mpaka sasa.

Kutopata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Madrid kwa muda sasa, ni kati ya sababu zinazomfanya kiungo huyo kuwa kwenye nafasi ya kutafuta timu nyingine ya kuichezea na kuondoka kabisa Hispania ambapo ameitumikia Madrid tangu 2013.

Mkataba wa kiungo huyo unaisha 2023 lakini kwa mujibu wa wakala wake ambaye pia ni baba yake – Francisco Alarcon alisema mchezaji huyo anatafuta timu nyingine lakini pia hatokuwa na tatizo kama atahitajika kuendelea kubaki Madrid.

“Kwa sasa hatujapokea ofa yeyote lakini Isco anataka kujaribu ligi nyingine. Kubaki Madrid haitokuwa na tatizo pia.” alisema Francisco wakati akizungumza na Cadena SER jana (Jumatatu)

Tangu mchezaji huyo amejiunga na Madrid, ameshinda makombe 2 ya La Liga na 4 ya Ligi ya Mabingwa. Everton, Arsenal na Manchester City ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuwania saini ya kiungo huyu raia wa Hispania.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

24 MAONI

  1. Sio mbaya akiondoka ingawa hasaivi ninaona wachezaji wanataka kupewa nafasi kucheza sana hivyo kama akikosa huwa wanataka kuondoka kumbe hata huko wanapo taka kwenda nako pia kina ambao wanataka kuondoka au kwa sababu ya uchumi unalipwa kotokana na kazi yako uliyo ifanya au ni maneno ya wahenga kila mtu anariziki yake huo niuwamuzi wako tu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa