Mkurugenzi mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amebainisha kuwa itakuwa “heshima” kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah lakini anasema kuwa hawana mpango wowote wa kumleta Ujerumani.
Salah, ambaye alijiunga na Liverpool kutoka Roma ya Italia mnamo 2017, amekuwa bora zaidi chini ya Jurgen Klopp na kuwa mmoja wa washambuliaji bora ulimwenguni, licha ya kushindwa kufanikiwa Chelsea mapema mwanzoni mwa soka lake.

Uchezaji wa Mmisri huyo umevivutia vilabu vingi vikubwa barani Ulaya huku Rummenigge akimtazama nyota huyu mwenye umri wa miaka 28, akimlinganisha na wachezaji kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, hata hivyo hatarajii Salah kuwasili katika kilabu cha Bundesliga wakati wowote hivi karibuni.
“Kwa maoni yangu, Salah ndiye Messi wa Afrika na kwa kweli ana ujuzi wa kucheza kwa timu bora ulimwenguni,” Rummenigge alizungumza na ON Time Sports.
“Alichofanikiwa kinaweza kulinganishwa na kile ambacho Messi na Ronaldo walifanya na Barcelona na Real Madrid.
“Kwa sasa hatuna mpango wa kumsaini Salah, lakini kwa kweli itakuwa heshima kuwa naye.”
Nyota huyo kwa sasa ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu, akicheka na nyavu mara 16 katika mechi zake 22 hadi sasa kwenye kampeni ya msimu huu.
Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.




Caroline
Sallah ni kiungo mzuri sana
Magdalena
Liverpool wakimuachia Salah watakuwa wamevurugwa sana
Sadick
Salah ni mshambuliaji mahiri kwa sasa ndani ya kikosi cha Liverpool,sidhani kama anaweza kupata mafanikio mahali pengine
Sarah
Dallas Yuko vizuri
Rahma
Salah baba lao
Hopemwaikuka
Kwenye kuhama liver hapo mbona kama kipengele
Dorophina
Sidhani kama liverpool watakubali kumuachia jembe salah
Mwanahamisi
Dallas Yuko poa
Angelina
Salah yuko vizuri
Sania
Salah baki nyumbani kumenoga
Lydia Emmanuel Magoti
Salah yupo vizuri
Issa
Salah bado
warda
Salah mwenyew kama Messi full mashauzi