Timu ya Taifa ya Italia imeanza vyema katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya EURO 2020 kwa ushindi mnono wa goli 3-0 dhidi ya Uturuki.

Italia inayonolewa na Roberto Mancini ilionyesha kiwango bora katika mchezo wa kwanza wa kundi A unaohusisha timu za Uturuki, Italia, Wales na Switzerland.

 

italia, Italia Waanza Kibabe EURO 2020., Meridianbet

Gli Azzurri walianza kujipatia goli kupitia kwa beki wa Uturuki Merih Demiral aliyejifunga dakika 53′ ya mchezo, kabla ya Immobile kuongeza dakika ya 66′ na kapteni Insigne kufunga orodha hiyo dakika ya 79′.

Ni kwa mara ya kwanza The Blues katika mechi 39 za kimataifa ambayo timu hiyo imefanikiwa kufunga magoli zaidi ya mawili katika mechi.

Mara ya mwisho kikosi cha Mancini kufungwa ni mwaka 2018 walipopoteza 1-0 dhidi ya Portugal katika mashindano ya UEFA National League. Mpaka sasa hawajapoteza katika michezo 28 ya kimataifa wakishinda mara 23 na sare 5.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa