Italia: Wachezaji Watasaini Vilabu Vitatu Msimu Mmoja

Kutoka Italia, wachezaji sasa wataruhusiwa kusainiwa na klabu tatu katika msimu mmoja. Shirikisho la Soka Italia (FIGC) wamekubaliana na kujumuisha kwenye taratibu zao kuwa wachezaji wanaweza kuwakilisha vilabu zaidi ya viwili.

FIGC wameungana na maamuzi ya FIFA kuwa wachezaji waruhusiwe kuwakilisha timu tatu zaidi ya mbili katika msimu mmoja kama ilivyokuwa awali.

Italia: Wachezaji Watasaini Vilabu Vitatu Msimu Mmoja

Maamuzi haya awali yalifanyika na FIFA mwezi Juni, katika kutafuta njia mbadala ya kuendana na athari za Virusi vya Corona ambazo kwa kiasi kikubwa zinapelekea mabadiliko makubwa ya mara kwa mara kwenye mechi, huku timu zikiwa na mizigo ya kukimbizana na ratiba ngumu ya mechi nyingi.

Chama cha Wachezaji Italia (AI) pamoja na Shirikisho la Soka Italia (FIGC) wametangaza kuwa utaratibu huu utaanza kutumika kwenye dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Kwa maana hiyo, ikiwa sheria hii inaanza kutumika, basi kuanzia mwezi Januari, wachezaji wataweza kusainiwa kuwakilisha vilabu vitatu katika msimu mmoja.

VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

16 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

    Wataweza kweli

    Jibu

    Litakuwa Ni jambo zuri

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

    Jambo jema

    Jibu

    Habari nzuli

    Jibu

    Kama inawezekana fresh tu

    Jibu

    Hii itakua nzuri sana

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Hii ipo vizuri sana itawasaidia wachezaji

    Jibu

    Maamuzi haya awali yalifanyika na FIFA mwezi Juni, katika kutafuta njia mbadala ya kuendana na athari za Virusi vya Corona ambazo kwa kiasi kikubwa zinapelekea mabadiliko makubwa ya mara kwa mara kwenye mechi, huku timu zikiwa na mizigo ya kukimbizana na ratiba ngumu ya mechi nyingi.

    Jibu

    Ni jambo jema kiukweli

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

Acha ujumbe