Ivan Toney Aingia Kwenye Rada za Spurs

Mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney raia wa kimataifa wa Uingereza ameingia kwenye rada za klabu ya Tottenham Hotspurs katika majira haya ya joto.

Klabu ya Tottenham inapambana kuhakikisha inapata mshambuliaji wa viwango sokoni katika majira haya ya joto kwajili ya kuboresha kikosi chao msimu ujao, Ivan Toney ni moja ya majina ambayo yanatawala katika orodha ya washambuliaji wanaofuatiliwa kwa karibu na klabu ya Spurs.ivan toneyKlabu hiyo kutoka London Kaskazini msimu uliomalizika haikua na msimu mzuri na moja ya maeneo ambayo yalichangia kuwarudisha nyuma ni eneo la ushambuliaji, Kwani klabu hiyo ni moja ya timu zilizotengeneza nafasi nyingi lakini hazikua zinatumiwa kwakua walikosa mshambuliaji mzuri.

Klabu ya Tottenham inataka kuhakikisha inapata mshambuliaji mwenye ubora mkubwa katika majira haya ya joto na ndio maana inahusishwa na kwa karibu  na mshambuliaji Ivan Toney pamoja na Dominik Solanke wa Bournamouth, Hii inaonesha kwa kiwango gani klabu ya Tottenham inahitaji kupata mshambuliaji mwenye ubora.

Acha ujumbe