Mchezaji wa Brentford Ivan Toney ametwaa tuzo ya goli bora la mwezi Septemba ambapo goli hilo limetokea kwenye mechi yao waliyocheza dhidi ya Leeds na wao kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Mechi hiyo iliisha huku Ivan Toney akiingia kambani mara tatu (Hattrick) huku goli la kwanza akifunga kwa mkwaja wa penati dakika ya 30, huku dakika ya 64 Leeds wakipata adhabu ya kadi nyekundu.
Mchezaji huyo amekuwa na kiwango kizuri sana toka wapande ligi kuu huku timu yao ikipewa jina la “Nyuki” kutokana na kasi waliyonayo ya kukimbia na kushambulia lango la mpinzani.
Frank Thomas ambae ni kocha wa timu hiyo ametoa kipigo kikubwa kwa Manchester United cha mabao 4-0 huku mpaka sasa wakishikilia nafasi ya 9 baada ya mechi zao 7 walizocheza. Brentford imekuwa timu ambayo inatoa changamoto kubwa hasa kwa vilabu vikubwa na vingine.
Ivan Toney amekuwa mchezaji anayevutia kumtazama kwenye timu hiyo kutokana na kiwango chake ambacho alimshawishi hadi kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza kumuita kwenye kikosi cha England kitakachoriki Kombe la Dunia Qatar mwezi Novemba.