Ivan Toney Kutimkia Saudia

Mshambuliaji wa klabu ya Brentford na timu ya taifa ya Uingereza Ivan Toney anahusishwa kwa karibu na kujiunga na vilabu vya Saudia Arabia ambavyo vinaelezwa kumpa ofa nono.

Ripoti mbalimbali zimeeleza kua mshambuliaji Ivan Toney anawindwa na vilabu kadhaa kutoka nchini Saudia ambavyo vinashiriki ligi kuu nchini humo, Mpaka sasa wako kwenye mazungumzo na mchezaji huyo halikadhalika klabu yake ya Brentford inatambua juu ya suala hilo.ivan toneyMshambuliaji huyo leo hakua sehemu ya kikosi ambacho kimecheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Crystal Palace na kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja, Kocha wa klabu hiyo Thomas Frank akikiri kuna suala la linaendelea kwa mchezaji huyo ndio maana wameamua kutokumueka kwenye kikosi leo.

Kocha Thomas Frank ameeleza pia pamoja na suala hilo kuendelea lakini bado halijakamilika mpaka sasa hivo bado klabu ya Brentford wanaweza kua na nafasi ya kumbakiza mshambuliaji wao nyota Ivan Toney, Au mshambuliaji huyo akaamua kukubaliana na ofa hizo kutoka Saudia Arabia na kutimkia huko.

Acha ujumbe