James Maddison ameendelea kumuonesha kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gary Southgate kua hayupo sahihi kwa kuacha kumuita kwenye kikosi chake cha timu ya taifa hilo.

james maddisonKumekua na mijadala mingi kua kiungo huyo anayekipiga katika klabu ya Leicester City anastahili kuitwa na kupewa nafasi kwenye timu ya taifa ya Uingereza chini ya kocha Southgate ambaye amekua hamuiti kiungo huyo kwenye kikosi chake mara kwa mara.

James Maddison licha ya klabu yake ya Leicester kutokufanya vizuri amekua na kiwango bora sana kwenye timu hiyo jambo linalofanya watu wengi kuhoji kwanini hapati nafasi timu ya taifa ya Uingereza.

Hali imechafuka tena na kurudisha mjadala huu baada ya jana usiku Kiungo huyo kuisaidia timu yake kushinda magoli manne kwa bila dhidi ya Nottingham Forest na yeye kuhusika magoli matatu kati ya manne baada ya kufunga magoli mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Baada ya James Maddison kuonesha ubora wa hali ya juu usiku wa jana imeibua mijadala tena na wadau webgi kusema itakua aibu kwa kocha huyo kumuacha mchezaji huyo kwenye kikosi chake kitakachoelekea Qatar kwenye michuano ya kombe la dunia mwezi novemba.

james maddisonBaada ya jana Maddison kufunga magoli mawili na kupiga pasi moja ya bao anakua mchezaji wa pili aliyehusika kwenye magoli mengi tangu mwezi Mei kwenye ligi hiyo akiwa amehusika kwenye magoli 14 akiwa nyuma ya Earling Haaland aliehusika kwenye magoli 17.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa