James Rodriguez mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid anakaribia kujiunga na klabu ya Olympiacos ya nchini Ugiriki.

James ambae alikua anaitumikia klabu ya Al- Rayyan ya nchini Qatar amefanya mazungumzo na klabu hiyo kongwe ya nchini Ugiriki na yupo kwenye hatua za mwishoni za kujiunga kwenye klabu hiyo na mchezaji huyo amesafiri kuelekea Ugiriki kukamilisha vipimo vya afya ili kujiunga na klabu hiyo kwani makubaliano binafsi yameshafikiwa baina ya klabu na mchezaji huyo.

james rodriguezNyota huyo wa zamani wa vilabu vya Porto,As monaco, Real madrid,Bayern munich pamoja na Everton amekua hana wakati mzuri toka aondoke ndani ya Real madrid akiwa amezunguka vilabu kadhaa ndani na nje ya ulaya.

Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia anakwenda kuungana na nyota mwezake wa zamani wa klabu ya Real madrid Marcelo Viera ambaye nae amejiunga na timu hiyo siku kadhaa nyuma.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa