Mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Jamie Carragher amesema kuwa kwa kiwango anachokionyesha hivi sasa mshabuliaji wa klabu ya Man Utd Marcus Rashford hapaswi kuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Marcus Rashford mwenye miaka 24 amekuwa na kiwango kibovu hivi karibuni lakini bado amekuwa kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya makocha Ralf Rangnick na Ole Gunnar Solskjaer, pia msimu huu amefanikiwa kuanza kwenye michezo 14 katika mashindano yote na kufanikiwa kufunga magoli matano na kusaidia mawili.

Pia alifanikiwa kuwepo kwenye mchezo Man Utd walipocheza na atletico madrid ambao walitoka sare, huku mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Paul Scholes akimkosoa kwa kusema anjaribu kufanya jambo la ajabu kila muda ambao anapopata mpira.

Jamie Carragher pia alieleza jinsi aanavyokatishwa tamaa na Rashford wakati akihoji kwa nini Rangnick asimuondoe kwenye kikosi cha kwanza.

“Marcus Rashford amekuwa kwenye timu tokea akiwa mdogo, amekuwa sehemu mchezo na mara zote amekuwa na shauku ya kupiga hatua, wanapokuwepo wachezaji wakubwa, yeye anakuwa bado yupoyupo tu.

“Tumefika hatua ambapo sidhani kama anapaswa kuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha Man Utd, kiwango chake msimu huu hakimuhakikishii kuwepo kwenye timu, amekuwa kwenye timu mara kwa mara, hata ambapo wachezaji wengine wanaoweza kucheza lakini watatafuta nafasi ya yeye kucheza.

“Lakini tunasubili Rashford kuweza kuifanya klabu ya man Utd makubwa au mchezaji atakayeweza kuifanya klabu hiyo kubeba makombe makubwa lakini bado rashord hajafikia hapo.” Jamie Carragher aliongezea.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa