Jamie Carragher asema safu ya ulinzi ya Liverpool kuwa “inatia aibu” hii ni baada ya kichapo cha 2-1 dhidi ya Manchester United, huku Gary Neville akisifu timu yake ya zamani kwa kuonyesha “vita, ari na nguvu” baada ya kuanza vibaya msimu huu.

carragher, Jamie Carragher: Liverpool Safu ya Ulinzi Inatia Aibu, Meridianbet

Baada ya kuanza vibaya msimu mpya kwa timu zote mbili, ni United ambao walionyesha kiwango cha kuvutia Old Trafford na kutwaa pointi tatu kwa kustahili na kumhakikishia Erik ten Hag ushindi wake wa kwanza kama kocha mkuu licha ya Liverpool kuonekana kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa lakini walishindwa kutumia nafasi zao kutengeneza magoli.

carragher, Jamie Carragher: Liverpool Safu ya Ulinzi Inatia Aibu, Meridianbet

Jadon Sancho alitangulia kufunga kipindi cha kwanza kwa kumalizia vyema kabla ya Marcus Rashford kuifungia United bao la pili baada ya mapumziko. Mohamed Salah alirudisha bao dakika za mwisho, lakini wenyeji wakashikilia ushindi huo wa kuongeza morali.

carragher, Jamie Carragher: Liverpool Safu ya Ulinzi Inatia Aibu, Meridianbet

United ilichakazwa na kufedheheshwa kwa mabao 4-0 wikendi iliyopita dhidi ya Brentford, lakini ni kikosi cha Jurgen Klopp ambacho kilionekana kuwa hatarini kwa ulinzi Jumatatu usiku na Carragher hakusita kutoa tathmini yake.

“Liverpool walishangaza sana kwenye kujilinda, Hawakuwa kwenye ushindani kabisa, Kila wakati United ilishambulia walionekana kama wangefunga, ilikuwa ni aibu. Liverpool walikuwa wamejaa kila mahali, United walikuwa bora, lakini Liverpool hawakuwa tayari kwa mchezo wa derby, hawakuonekana kuwa tayari kwa mchezo”. Carragher alisema.

Neville: Ninajivunia Man Utd

Kwa upande wa Man UTD, ushindi huo unaifanya timu hiyo kuwa juu ya Liverpool kwenye msimamo wa Ligi, ambapo Neville alifurahishwa na lakini akashangazwa na uchezaji wao.

carragher, Jamie Carragher: Liverpool Safu ya Ulinzi Inatia Aibu, Meridianbet

“Ninajivunia kama shabiki wa Manchester United kuwatazama wachezaji hawa na sikuwahi kufikiria ningesema hivyo baada ya wiki chache zilizopita, jinsi walivyopambana, ari na nguvu kutoka kwa Manchester United ilikuwa nzuri”. Alisema Neville

Keane: Man Utd wanastahili sifa zote

Nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane aliongeza:

carragher, Jamie Carragher: Liverpool Safu ya Ulinzi Inatia Aibu, Meridianbet

 “Kuingia kwenye mchezo huku kocha akiwaweka nje Maguire na Cristiano Ronaldo, na wachezaji waliitikia kwakweli walikuwa bora. Ni nguvu kubwa kwa Ten Hag, itampa kila mtu nguvu na hali ya kujisikia vizuri itarejea kwa siku chache. Walistahili kukosolewa wiki iliyopita lakini walikuwa bora sana wanastahili sifa zote.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa