Kwa mujibu wa mgombea uraisi wa Barcelona Joan Laporta, staa wa klabu hiyo Lionel Messi anahitaji zaidi mapenzi kutoka kwa timu na mashabiki na kushinda mataji na sio pesa.

Pesi amekuwa akihusishwa zaidi na kuhamia mabingwa wa Ligue 1, Paris Saint Germain na miamaba ya Ligi Kuu Uingereza Manchester City, tangia alipojaribu kuwasilisha ombi lake la uhamisho mwaka jana.

Sakata la hatma ya Messi na Barcelona linaendelea kuwa kitendawili, ambacho kinaweza kujibika pale Messi atakapofanya maamuzi ya hatma yake.

Hata hivyo, kwa mujibu Joan Laporta, ambaye anagombea Uraisi wa klabu hiyo, anasema kuwa Messi hahitaji kabisa hamasa ya pesa, isipokuwa ni kupendwa na kushinda mataji.

Joan Laporta: Messi Anahitaji Kupendwa na Mataji

Laporta ameitaja kuwa historia ya mapenzi ya Mesii kwa Barcelona ni historia nzuri sana na kwa mtazamo wake hiyo ndiyo ilipaswa kupaliliwa ili kumpa hamasa zaidi nyota huyo zaidi ya kufikiria kuwa pesa nidyo inaweza kumbadilisha.

“Anatakiwa kupendwa. Anastahili hilo. Na anahitaji kuthaminiwa kwa ofa bora ya kiuchumi ambayo itamfanya aione thamani yake, lakini haendeshwi na pesa.”

Laporta, ambaye anasema anamfahamu vyema Messi na wana uhusiano mzuri, anaamini kuwa atapata nafasi ya kufanya kila awezalo kumshawishi Messi kusalia Barcelona.

“Ni mshindi. Anachohitaji ni kushinda tena na Barcelona. Nitaenda kufanya kila niwezalo kumbakiza hapa.”


 

WEWE NI SHUJAA? MASHUJAA WANASHINDA HAPA!

Treasure Heroes inakupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

Kasino ya Mtandaoni

INGIA MCHEZONI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa