Mchezaji mpya wa Chelsea ambaye amesajiliwa kwa mkopo kutoka Atletico Madrid Joao Felix ameanza vibaya Ligi kuu ya Uingereza baada ya kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo wake wa kwanza jana.

 

Joao Felix Aanza na Bahati Mbaya ya Kukosa Mechi 3 za Chelsea Zijazo

Joao Felix alipewa kadi hiyo katika kipindi cha pili dakika ya 58 baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Fulham Kenny Tete kwenye mchezo ambao The Blues walipoteza kwa mabao 2-1.

Chelsea sasa ipo katika kipindi kigumu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Carabao Cup, FA, Kumaliza nafasi nne za juu ni ngumu kutokana na kuwa anazidiwa pointi takribani 10 na aliyepo nafasi ya 4 United.

Joao Felix Aanza na Bahati Mbaya ya Kukosa Mechi 3 za Chelsea Zijazo

Vijana wa Potter wamebakiza Ligi ya Mabingwa peke yake mpaka sasa ambayo itaanza February 15 watakapomenyana dhidi ya Borussia Dortmund huko Signal Iduna Park mwaka huu.

Chelsea mpaka sasa katika mechi 10 za ligi amaeshinda mbili pekee kitu ambacho msimu uliopita hakikuwepo na mpaka January hii anashikilia nafasi ya 10 huku hata uwezekano wa kucheza michuano ya Europa ukiwa mdogo.

Joao Felix Aanza na Bahati Mbaya ya Kukosa Mechi 3 za Chelsea Zijazo

Joaa Felix atakosa mechi ya Crystal Palace hapo kesho, Liverpool, pamoja na mechi ya Fulham itakayopigwa pale darajani.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa