Joao Pedro Avunja Laana ya Namba 9 Chelsea kwa Sekunde 31 Tu

Joao Pedro hakuhitaji muda mrefu kuanza kuandika ukurasa mpya akiwa na jezi namba tisa ya Chelsea, akitumia sekunde 31 pekee kuonyesha kwamba hana hofu na kile mashabiki wa klabu hiyo wanachokiita laana ya namba 9. Mshambuliaji huyo wa Brazil alitumia ustadi wa hali ya juu kuuinua mpira juu ya kipa wa Fulham, Bernd Leno, na kuifungulia Chelsea njia kuelekea ushindi wa kusisimua wa mabao 3-2 huko Craven Cottage.

Joao Pedro Avunja Laana ya Namba 9 Chelsea kwa Sekunde 31 Tu

Ushindi huo ulikuwa wa kipekee zaidi kwa sababu ulikuwa mchezo wa kwanza wa Xabi Alonso akiwa kocha wa Chelsea, huku Joao Pedro akiwa moja ya mastaa walioangaza zaidi. Mwishoni mwa wiki iliyopita, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipewa rasmi jezi namba tisa pamoja na mkataba mpya ulioboreshwa kifedha ambao utamfanya kubaki Chelsea hadi mwaka 2034. Hata hivyo, pamoja na heshima hiyo kubwa, namba hiyo imekuwa ikibeba kumbukumbu zisizo nzuri kwa baadhi ya mashabiki wa Chelsea, ambao wanaamini kuwa imekuwa na laana kwa wanaoivaa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Tangu Jimmy Floyd Hasselbaink kuondoka Chelsea mwaka 2004, hakuna mshambuliaji aliyefanikiwa kwa kiwango kikubwa akiwa amevaa namba hiyo. Didier Drogba aling’ara akiwa na namba 11, huku Diego Costa akifanya mambo makubwa akiwa na namba 19. Lakini majina makubwa kama Romelu Lukaku, Alvaro Morata, Gonzalo Higuain, Radamel Falcao na Pierre-Emerick Aubameyang yalipitia kipindi kigumu Stamford Bridge wakiwa wamevaa namba tisa. Liam Delap, ambaye ndiye aliyekuwa mmiliki wa mwisho wa jezi hiyo kabla ya Joao Pedro, naye alifunga bao moja pekee la Premier League msimu uliopita.

Joao Pedro Avunja Laana ya Namba 9 Chelsea kwa Sekunde 31 Tu

Lakini Joao Pedro hana mpango wa kuamini simulizi hizo. Baada ya kufunga dhidi ya Fulham, alipohojiwa kuhusu laana hiyo, alisisitiza kwamba haamini namba inaweza kuamua kiwango au presha ya mchezaji. Na kwa takwimu zake, ana sababu ya kujiamini. Msimu uliopita alifunga mabao 20 katika mashindano yote, akilingana na namba yake mpya ya jezi na kuwa mshambuliaji wa kwanza wa Chelsea kufikisha idadi hiyo tangu Diego Costa afanye hivyo miaka tisa iliyopita.

Joao Pedro Avunja Laana ya Namba 9 Chelsea kwa Sekunde 31 Tu

Chelsea iliwalipa Brighton pauni milioni 55 pamoja na bonasi zinazoweza kufikisha pauni milioni tano ili kumsajili Joao Pedro msimu uliopita, na sasa klabu inaamini kabisa kuwa uwekezaji huo unaanza kulipa. Watu walio karibu na mshambuliaji huyo pia wanaamini ametimiza kile alichostahili baada ya safari yake ya kupanda hadi kileleni mwa soka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.