Joao Pedro mchezaji nyota wa klabu ya Watford amefanikiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Uingereza maarufu kama Championship.

Mchezaji huyo raia wa Brazil amesaini kandarasi mpya klabuni hapo mpaka mwaka 2028 kusalia klabuni hapo, mchezaji huyo ambaye alikaribia kujiunga na klabu ya Newcastle lakini dili hili lillishindwa kufanikiwa mwishoni kabisa.

Mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa baada ya kusaini mkataba huo mpya inaelerzwa mshahara umeongezwa na maboresho mengine yakiwepo.

joao pedroKusaini mkataba mpya kwa kinda huyo mwenye umri wa 21 na kipaji kikubwa kwenye timu hiyo inayoshikiri ligi daraja la kwanza nchini Uingereza kimewashangaza watu wengi kwani kwa kipaji cha mchezaji huyo ni cha kucheza kwenye vilabu vya hadhi ya juu na kushiriki michuano mikubwa.

Lakini hii inaweza akili ya kibiashara kwa klabu ya Watford ambao wamempa mkataba mrefu kinda huyo mwenye kipaji ilhali wanajua hatakua na maisha marefu klabuni hapo ili waweze kupata pesa ya kutosha kwa timu itakayomuhitaji mbeleni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa