Mchezaji mkongwe zaidi wa Real Betis Joaquin ameweka jina lake katika historia ya ligi ya Europa baada ya kuwa mfungaji mwenye umri mkubwa katika shindano hilo kwa bao la kipindi cha kwanza dhidi ya Ludogorets.

 

Joaquin Aweka Rekodi Europa

Vijana hao wa Manuel Pellegrin walikuwa mbele baada ya dakika 25  hapo jana kufuatia  Luiz Enrique kuunganisha kwa kichwa krosi ya Juan Miranda. Nahodha Joaquin aliiongezea Betis faida mara mbili dakika 6 kabla ya kipindi cha mapumziko baada ya kupata mpira wa kona uliopigwa.

Bao hilo lilimfanya Joaquin, mwenye umri wa miaka 41 na siku 56 kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao kwenye michuano ya Europa, na kumpita Daniel Hestade wa Molde baada ya bao lake dhidi ya Celtic November 2015.

 

Joaquin Aweka Rekodi Europa

Real Betis wamekuwa na mwanzo mzuri msimu huu kwenye ligi ya Laliga ambapo wamekuwa wakileta ushindani kwani mpaka sasa wapo nafasi ya tatu ya msimamo baada ya kucheza michezo mitano, huku wakishinda michezo  minne hawana sare na wamepoteza mchezo mmoja na wamejikusanyia alama 12 wakiwa nyuma ya alama tatu dhidi ya anayeongoza ligi ambaye ni Real Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa