John Obi Mikel Atua Rasmi Stoke City.


Stoke City inayoshiriki Ligi ya Daraja la Kwanza nchini Uingereza (Championship) imemsajili nahodha wa zamani wa Super Eagles ya Nigeria, John Mikel Obi, 33 kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mikel ambaye pia amewahi kuvalia jezi za Chelsea, alisalia bila klabu baada ya kuagana rasmi na Trabzonspor ya Uturuki mnamo Machi 2020.

Kusajiliwa kwa Mikel kunatokea siku mbili baada ya kukiri kwamba alikuwa radhi zaidi kurejea kusakata soka ya Uingereza.

 

John Obi Mikel Atua Rasmi Stoke City.

Akiwa mwanasoka wa EPL, Mikel aliwajibishwa na Chelsea mara 249 katika kipindi cha miaka 11.

Aliondoka uwanjani Stamford Bridge mnamo 2017 baada ya kushindia waajiri wake ufalme wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), mataji mawili ya EPL, makombe matatu ya FA na taji moja la Carabao League Cup.

Baadaya kukatiza uhusiano na Chelsea, aliyoyomea China kuvalia jezi za Tianjin TEDA kabla ya kuingia katika sajili rasmi ya Middlesbrough nchini Uingereza kwa kipindi kifupi mnamo 2019.

Hadi alipotangaza kustaafu rasmi kwenye soka ya kimataifa, Mikel alikuwa amewajibishwa na timu ya taifa ya Nigeria mara 89.

 

John Obi Mikel Atua Rasmi Stoke City.

Aliongoza kikosi hicho cha Super Eagles kwenye fainali mbili za Kombe la Dunia na akakisaidia kunyanyua ubingwa wa Kombe la Afrika (AFCON) mnamo 2013 nchini Afrika Kusini.

Stoke City walisajili ushindi kwenye mechi tatu kati ya nne za mwisho katika kivumbi cha Championship msimu huu wa 2019-20 na kukwepa shoka ambalo vingnevyo lingewateremsha ngazi hadi Daraja la Pili (League One).

Kikosi hicho kiliambulia nafasi ya 15 chini ya kocha wa zamani wa Ireland Kaskazini, Michael O’Neill.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma Zaidi

42 Komentara

    Habari njema sana

    Jibu

    Atawasaidia sanaa maana jamaa anajua sanaa

    Jibu

    Maoni:vizuri asaidie stoke iweze ludi EPL

    Jibu

    jamaa anawajua atawasaidia

    Jibu

    Safiii sana jembe

    Jibu

    Mikel Obi anakumbukwa darajani kwa uwezo wake wa kukaba zaidi hakuwa na uwezo wa kupiga pasi kusaidia timu kupata goli#meridianbettz

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Karibu tena England Mr obi

    Jibu

    Habar njma kwa stoke city

    Jibu

    Makala nzur asante kwa iyo

    Jibu

    Jamaa yupo vizuri

    Jibu

    hizi ni habari njema kwa stoke city

    Jibu

    Kila la kheri Mikel obi katika Misha mapya ndani ya stoke city

    Jibu

    Nenda kapambane#meridianbett

    Jibu

    All the best

    Jibu

    Makini sna

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    John Mikel Obi ni mchezaji mzur sana

    Jibu

    Hongera sana stoke City wamempata mchezaji mzuri

    Jibu

    Jong namkubal sana

    Jibu

    Kila la kheri John

    Jibu

    Obi mikel ni safi kujiunga huko

    Jibu

    Mkongwe huyo kutokana na uzoefu wake wa mda mrefu ni msaada tosha kwa stoke city.

    Jibu

    Kila la kheri MUHENGA obi Mikel ss mashabik wako tunakudai kwny soka bado

    Jibu

    Good

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Imekaa poa

    Jibu

    Habari njema sana#Meridianbettz

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Kila la kher

    Jibu

    Naona Obi anamalizia ,alizia soka lake sasa

    Jibu

    Habari njema sana

    Jibu

    Mikel Ni talent player atawafaa

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Yupo vizuri sana john obi

    Jibu

    Yuko vizuri sana napia naamini atawasaidia mnoo

    Jibu

    Jamaa yupo vizuri

    Jibu

    nice

    Jibu

    Hongera sana.

    Jibu

    Mwamba bad yupo yup san

    Jibu

    City wamepata Kifaa

    Jibu

    Mikel anaenda kufanya maajabu huko stoke city na kuonyesha uwezo wake

    Jibu

Acha ujumbe