John Terry Ajiandaa Kurudi Chelsea

Beki kisiki wa zamani wa klabu ya Chelsea John Terry anajiandaa kurudi tena kwenye klabu yake ya zamani baada ya miaka mitano kuchukua mikoba ya kuwa kocha wa timu ya vijana.

John Terry mwenye miaka 41 aliachana na klabu ya Chelsea na kutumia muda huo kufanya kazi za ukufunzi huku akitumia muda wa miaka mitatu kwenye klabu ya Aston Villa akiwa kama kocha msaidizi wa Dean Smith kabla ya kuondoka majira ya kiangazi.

John Terry

Kapteni huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuachana na klabu ya Aston Villa alizunguka nchi mbalimbali za Ulaya akijifunza aina tofauti ya mifumo ya ukocha na kusubiri kazi mpya ya ukufunzi itakayopatikana.

Baada ya kuona wachezaji wenzie wa zamani kama Wayne Rooney, Frank Lampard na Steven Gerrard wakianza kufanya kazi zao kwa mara ya  kwanza nje ya ligi kuu ya Uingereza, Terry nae anaamini anaweza kupitia njia hiyo pia.

John Terry

Kwa sasa John Terry anaishi karibu na uwanja wa mazoezi wa Cobham na ameripotiwa kuwa na ukaribu na wachezaji wenzie wa zamani Petr Cech and Carlo ambao wamepata kuajiriwa na klabu ya Chelsea pia inesemekana mkurugenzi wa akedemi Neil Bath anamsaidia ili aweze kurejea tena kwenye klabu hiyo.


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.