Johnny Evans Kupewa Mkataba Mpya United

Beki wa klabu ya Manchester United Johnny Evans yupo kwenye nafasi ya kupewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa mwaka mwingine zaidi.

Johnny Evans mwenye umri wa miaka (35) katika hali ya kushtua klabuni hapo bado anapewa nafasi ya kuongezewa mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mashetani wekundu kwa msimu ujao.johnny evansIkumbukwe beki huyo alijiunga klabuni hapo msimu uliomalizika akitokea klabu ya Leicester City kwa uhamisho huru na kupewa mkataba wa mwaka mmoja ambao umemalizika tayari, Lakini mashabiki wa klabu hiyo hawaoni kama ni sahihi kw aklabu hiyo kumuongezea mkataba mchezaji huyo.

Beki huyo licha ya umri wake kua mkubwa lakini pia amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yanakua yanamueka nje ya uwanja kwa muda mwingi, Hivo mashabiki wa klabu hiyo wakiwa hawajaridhishwa kwa kiwango kikubwa na maamuzi ambayo klabu hiyo inataka kufanya.johnny evansKlabu ya Manchester United inaelezwa inatazamia kuingia sokoni kusajili beki wa katikati, Lakini mazungumzo ya mkataba mpya kwa Johnny Evans bado yanaendelea.

Acha ujumbe