Jonny Evans Asaini Mkataba Mpya Man United 2025

Beki wa klabu ya Manchester United Jonny Evans amefanikiwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo baaada ya kumalizika kwa mkataba wake msimu uliomalizika.

Beki huyo amejiunga na timu hiyo baada ya klabu ya Leicester City kushuka daraja msimu wa 2022/23 na kupata fursa ya kucheza ndani ya Man United kwa mara nyingine baada ya kuondoka klabuni hapo kw amuda mrefu na kujiunga na Man United.jonny evansNi wazi Jonny Evans ataendelea kubaki ndani ya klabu ya Man United mpaka mwaka 2025 baada ya kupewa mkataba wa mwaka mmoja msimu uliomalizika na mwaka huu ameongezewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja wa kuwepo ndani ya viunga vya Old Trafford.

Beki Jonny Evans ikumbukwe ameshawahi kuitumikia klabu ya Man United kwa kipindi fulani kwani beki huyo ameibuliwa kutoka kwenye akademi ya klabu hiyo, Inaelezwa beki huyo hajaongezewa mkataba kwasababu atacheza sana ndani ya timu hiyo lakini sababu kubwa ni kuleta motisha kwa wachezaji ndani ya timu hiyo haswa vijana wadogo.

Acha ujumbe