Staa wa zamani wa Kikapu wa NBA, Michael Jordan, MJ amezungumzia mawasiliano ya mwisho ya ujumbe wa maandishi na Kobe Bryant kabla ya kifo chake.

Akizungumza na EPSN, MJ aliongelea ujumbe wa mwisho baina yao ambayo walizungumza siku 49 tu kabla ya Kobe kufariki katika ajali ya helikopta ambayo pia alikuepo binti yake wa miaka 13 Gianna.


 

Baada ya Jordan kutuma chupa ya Cincoro Tequila yake mpya kwa Kobe kujaribu tena mnamo Desemba 2019, Legend huyo wa Los Angeles Lakers alimshukuru kwa kutuma ujumbe: “Tequila hii ni ya kushangaza.”

MJ: “Asante, ndugu yangu.”

Kobe: “Ndio bwana. Familia nzuri?” Kobe alisema.

MJ: “Yote nzuri. Yako?”

Kobe: “Yote nzuri.”

MJ: “Likizo njema natarajia kutakutana hivi karibuni. Kocha Kobe ??!”

Kobe: “Ah, nitarudi kwako. Hey, kocha, nimekaa kwenye benchi (la timu ya mpira wa kikapu ya Gianna) hivi sasa, na tunaongoza timu hii. 45-8.”

Jordan aliiambia ESPN kwamba “alipenda maandishi hayo”.

“Inaonyesha hali ya ushindani wa Kobe,” akaongeza.

Bingwa huyo mara sita wa NBA, Jordan pia alizungumza katika ibada ya kumbukumbu ya Kobe na Gianna iliyofanyika katika Kituo cha Staples.

“Kobe Bryant alipokufa, sehemu ya mwili wangu ilikufa,” MJ aliongea akitokwa machozi.

“Hizo ndizo kumbukumbu tunazopaswa kuishi nazo na tunajifunza kutoka kwako. Nakuahidi kuanzia leo naendelea kuishi na kumbukumbu za kujua kwamba nilijaribu kumsaidia kaka yangu mdogo kwa kila njia niliyoweza.

“Tafadhali pumzika kwa amani, kaka mdogo.”


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA


13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa