Joshua Mutale, kiungo mshambuliaji wa Simba SC amewagawanya mabosi wa timu hiyo kutokana na wengine kuhitaji kuona anaondoka huku wengine wakihitaji kuona anabaki ndani ya kikosi hicho.

Joshua Mutale hakuwa kwenye mwanzo mzuri msimu wa 2024/25 kutokana na mechi ambazo alipewa nafasi kucheza chini ya kiwango.
Katika mechi za mzunguko wa pili Joshua Mutale amekuwa akifanya kazi kubwa pale anapopewa nafasi katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.
Ni yeye alifunga bao pekee kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane walipopoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 na kugotea nafasi ya pili.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Taarifa zinaeleza kuwa kumekuwa na mvutano wa mabosi wa timu hiyo wamekuwa wakivutana kwa kuwa wapo wanaodhani hataendeleza ubora na wengine wakiamini kwamba bado ana uwezo wakuendelea kuwa kwenye ubora kwa msimu ujao.
Ni benchi la ufundi ripoti yao itaamua kwamba Joshua Mutale abaki ndani ya kikosi ama asepe kwa ajili ya kupata changamoto mpya sehemu nyingine kwa mkopo.


