Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Bologna ya nchini Italia Joshua Zirkzee ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Manchester United mapema leo baada ya kukamilisha taratibu zote.
Joshua Zirkzee anajiunga na Man United kutokea klabu ya Bologna kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 42 ambazo inaelezwa zitalipwa ndani ya miaka mitatu, Huku Bayern Munich nao wakipata aslimia 50% ya mauzo ya mchezaji huyo kutokana na kipengele walichokieka wakati wanamuuza Bologna.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anakwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Man United akiungana na wachezaji kama Marcus Rashford, Rasmus Hojlund, Alejandro Garnacho ambao watasimamiwa kwa karibu na aliyekua mshambuliaji matata klabuni hapo Ruud Van Nistelrooy kuhakikisha wanafunga mabao ya kutosha ndani ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo dili lake lilikamilika siku ya Alhamisi na kusafiri ijumaa nchini Uingereza ambapo jana Jumamosi alifanikiwa kukamilisha vipimo vya afya ndani ya timu hiyo, Huku akisaini mkataba wa miaka mitano mapema leo huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.