Jovic Ndiye Mchezaji Mwenye Furaha Zaidi?

Luka Jovic amebainisha kuwa yeye ndiye mwanasoka mwenye furaha zaidi baada ya kuwa mchezaji wa Real Madrid.

Madrid wanatajwa kuwa wamelipa paundi milioni 60 kuinasa sahihi ya mshambuliaji huyu anayetoka Eintracht Frankfurt.

Staa huyu ambaye ni raia wa Serbia aliwafungia Eintracht Frankfurt magoli 10 kwenye ligi ya Europa akiwasaidia klabu hiyo kufikia nusu fainali kabla hawajatolewa na Chelsea kwenye mikwaju ya penati. Staa huyu amechapa jumla ya magoli 17 kwenye Bundasliga.

Akizungumzia furaha yake Alhamisi iliyopita, Jovic aliahidi kufanya bidii zaidi kwa mafanikio ya klabu.

“Mimi ni jamaa mwenye furaha zaidi duniani kusajiliwa na klabu kubwa kama hii. Nimefurahi sana, nina uhakika nilifanya uamuzi sahihi. Nitafanya kila niwezavyo kuisaidia Real Madrid kushinda mataji mengi zaidi.”

Zidane ameanza vyema kukijenga kikosi chake tayari kwa ajili ya msimu ujao, akiwa ameshawasogeza Eden Hazard, Eder Militao na Rodrygo Goes ndani ya kikosi tayari kwa mapambano.

Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez alipoteza matumaini na Real Madrid kadri ilivyofanya vibaya msimu uliopita. Anaamini Jovic na vijana wengine ambao tayari wameshamwaga wino klabuni hapo watawasha moto msimu ujao. Bila shaka watakuwa na kikosi bomba zaidi msimu ujao.

4 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Hongera kijana.

    Jibu

    Safi sana 👍

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

Acha ujumbe