Jude Bellingham Aifikia Rekodi ya Ronaldo

bellingham

Inaonekana kama stori ni ile ile, wiki tofauti kwa Jude Bellingham kwani aliweza kuifungia bao tena Real Madrid.

Mashabiki walishuhudia ubora wake akiwa na Birmingham City na Borussia Dortmund kabla ya kuhamia Santiago Bernabeu majira ya joto. Bellingham alifunga bao katika mechi yake ya kwanza ya Madrid wakishinda 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao kabla ya kufunga katika mechi tatu za LA LIGA mfululizo.

Ameonyesha mafanikio katika Ligi ya Mabingwa pia, akifunga dhidi ya Union Berlin na Napoli.

Kabla ya mechi dhidi ya Osasuna, Bellingham alikuwa amefunga magoli nane katika mechi tisa alizocheza kwa klabu.

Aliongeza idadi ya magoli zaidi siku ya Jumamosi alipofunga mara mbili katika ushindi wa 4-0. Bao la kwanza la Bellingham siku hiyo alipokea pasi kutoka kwa Dani Carvajal. Meridianbet inakupa odds kubwa mechi zote ikiwemo za LA LIGA.

Mpaka sasa Jude Bellingham ana magoli 10 katika mechi kumi za kwanza za akiwa na Real Madrid. Anakuwa mchezaji wa kwanza kufikia rekodi kama hiyo tangu msimu wa kwanza wa Cristiano Ronaldo mwaka wa 2009/10 wa mafanikio makubwa.

Bellingham pia yuko mbele ya nyota wa Barcelona, Robert Lewandowski, katika orodha ya wafungaji wa LA LIGA, akifunga magoli nane ikilinganishwa na matano ya Lewandowski. Meridianbet ina chaguo la kubashiri mfungaji bora wa mabao kwenye kila mechi na Ligi, chaguo hili lina odds kubwa. Bofya na Cheza.

Acha ujumbe