Julian Alvarez Akosa Mazoezi Atlético Madrid, Arsenal Yaendelea Kumfuatilia

Mshambuliaji wa Argentina, Julian Alvarez, hakushiriki katika mazoezi ya Atlético Madrid leo baada ya kujisikia vibaya usiku wa kuamkia leo, hali iliyomlazimu kubaki nyumbani kwa ajili ya kupumzika.

Julian Alvarez Akosa Mazoezi Atlético Madrid, Arsenal Yaendelea KumfuatiliaKwa mujibu wa taarifa kutoka Marca, Alvarez alipatwa na maumivu ya tumbo yaliyomsumbua kwa kiasi kikubwa usiku mzima, na hadi asubuhi bado hakuwa katika hali nzuri kiafya. Kutokana na hali hiyo, aliamua kutoshiriki mazoezi ya timu.

Mchezaji huyo anatarajiwa kutumia muda huu kupumzika ili kurejesha hali yake na kurejea mazoezini mara atakapokuwa amepata nafuu. Hakuna taarifa kwamba tatizo hilo ni kubwa au litamuweka nje kwa muda mrefu.

Julian Alvarez Akosa Mazoezi Atlético Madrid, Arsenal Yaendelea KumfuatiliaWakati huohuo, mustakabali wa Alvarez katika kikosi cha Atlético Madrid bado unaendelea kuzua mjadala, huku Arsenal ikiwa miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu na kusubiri uamuzi kuhusu hatua yake inayofuata.

Julian Alvarez Akosa Mazoezi Atlético Madrid, Arsenal Yaendelea KumfuatiliaHata hivyo, hadi sasa Alvarez hajaonyesha utayari wa kujiunga na klabu nyingine isipokuwa Barcelona, licha ya Atlético Madrid kuendelea kusimamia msimamo wake kuhusu mshambuliaji huyo wa Argentina.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.