Bado hali ni tete kuhusu hatma ya Georginio Wijnaldum ndani ya kikosi cha Jurgen Klopp kuanzia msimu ujao.

Mkataba wa Wijnaldum unamalizika mwishoni mwa msimu huu na mpaka sasa,maongezi ya mkataba mpya hayaoneshi dalili ya kuzaa matunda. Kufikia Januari 1, Georginio atakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu za nje ya EPL na ataondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu.

Sekeseke la mkataba mpya halimyumbishi Jurgen Klopp ambaye ameamua kuweka wazi adhma yake ya kumuhitaji Wijnaldum kwenye kikosi chake na angependa mchezaji huyo abaki Anfield.

Jurgen Klopp, Jurgen Klopp Anamuhitaji Wijnaldum, Meridianbet
Georginio Wijnaldum

Akizungumzia suala la mkataba mpya wa Wijnaldum ambaye anahusishwa sana na Barcelona. Jurgen Klopp amesema “Kiukweli siwezi kuliongelea sana hilo. Nitafurahi kama ataendelea kuwepo hapa. Ninafurahia kuwa na Gini kama ambavyo unawezakuona kwenye vikosi vingi.

“Anacheza vizuri kila mara, ndio maana ameshacheza idadi ya mechi ambazo ameshacheza mpaka sasa. Kusema kweli, sikumbuki idadi ya michezo ambayo amecheza vibaya.

“Anacheza katika nafasi nyingi kwenye kikosi chete, ni jambo la kumshukuru Mungu yupo kwenye hali nzuri na iendelee kuwa hivyo.

“Sijui amecheza mechi ngapi tangu nimekuja hapa, ni jambo jema na hakuna cha zaidi cha kusema katika hilo. Kutokana na kwamba hakuna kilichoamuliwa mpaka sasa, chochote kinaweza kutokea.”


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa