Makocha wa timu zote mbili Jurgen Klopp na Erik Ten Hag, walitoa maoni yao kuhusiana na mchezo wa jana huku kila mmoja akizungumza uchambuzi wake kitaalamu.

Jardon Sancho ndiye alikuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa Manchester United kwa goli tamu mithili ya mvinyo wa hekaluni, mpira ulioguswa na Bruno Fernandez ukamkuta Sancho akiwa kwenye nafasi nzuri. Alitumia akili kubwa kubwa na utulivu wa hali ya juu kuwachambua walinzi wa Liverpool na kuwaacha wamelalia nyasi za Dimba la Old Trafford, huku akiuzamisha mpira kiufundi kwenye nyavu za wapinzani.

klopp, Jurgen Klopp: Kama Tungecheza kwa Ubora Tungeshinda, Meridianbet

Haikuishia hapo, nae Marcus Rashford alitumia dakika chache tu kuweka goli la pili huku kwa shambulizi la kushitukiza, alipenya kama mshale na kumtoka beki wa Liverpool akiwa hajui nini cha kufanya, lakini baadae mnamo dakika ya 81 kijana kutoka nchi yenye mapiramidi mengi, Misri akasawazisha goli la kwanza na mpaka filimbi ya mwisho Man Utd walishinda goli 2-1.

klopp, Jurgen Klopp: Kama Tungecheza kwa Ubora Tungeshinda, Meridianbet

Makocha wa timu zote mbili walipata nafasi ya kuzungumza na kila mmoja alitoa mtazamao wake kutokana na mchezo huo, huku Ten Hag akionekana kusifia kiwango kilichooneshwa na vijana wake.

klopp, Jurgen Klopp: Kama Tungecheza kwa Ubora Tungeshinda, Meridianbet

“Tunaweza kuzungumza kuhusu mbinu lakini yote ni kuhusu mtazamo, Kulikuwa na mawasiliano na roho ya mapigano, niliwaambia wachezaji tunapaswa kuchukua hatua, sio kuzungumza sana, inanifurahisha Rashford na Sancho kufunga mabao. Aliongeza kwa kusema:

“Nimefurahishwa na upambanaji lakini lazima tuwe hivi kwenye kila mchezo na isiwe tu dhidi ya Liverpool. Kila mechi ya Ligi Kuu ni ngumu, tunahitaji kuileta kwenye kila mchezo”. Alisema Erik Ten Hag

Kwa upande wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kwamba kama wachezaji wake wangecheza kwenye ubora mkubwa basi matokeo ya ushindi yangekuwa upande wao.

klopp, Jurgen Klopp: Kama Tungecheza kwa Ubora Tungeshinda, Meridianbet

“Ni dhahiri tuko katika hali ngumu ya majeraha kwa wachezaji wetu baadhi, tunamaliza wiki nzima tukiwa na wachezaji 14-15 wakubwa, lazima tuhakikishe hakuna hata mmoja wao atakayejeruhiwa kwa sababu hakuna chaguo halisi lililobaki.

“Hata kwa hali yetu, lakini tumecheza vizuri kidogo, kama tungekuwa na umakini zaidi juu ya kile tunachofanya tungeshinda mchezo huu. Najua inaonekana ni ujinga, lakini ndivyo ninavyoona. Walikuwa hatari sana mwanzoni, ilikuwa wazi kabisa nini kitatokea, ukweli unaonyesha kama tuko tayari, na mwanzo walikuwa hatari kuliko sisi”. Klopp alisema.

Manchester United watawafata Southampton Jumamosi, na kisha  Vijana wa Erik ten Hag watasafiri hadi Leicester City Septemba 1, kabla ya kuwakaribisha Arsenal siku tatu baadaye. Unaweza kubashiri mechi hizo zote hapa #meridianbet

Liverpool sasa watakuwa na mechi mbili za nyumbani ya kwanza dhidi ya Bournemouth Jumamosi hii, kisha dhidi ya Newcastle Jumatano iliyofuata, na umakini utaelekezwa kwenye mchezo wa Merseyside derby dhidi ya Everton katika mechi ya Jumamosi ya mchujo Septemba 3.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa