Tamko la kuruhusu mashabiki kuhudhuria baadhi ya michezo ya EPL, limechukuliwa tofauti na kila mtu. Kwa Jurgen Klopp, hii “ni hatua kwenye uelekeo sahihi”.

Siku ya Alhamisi, serikali ya Uingereza ilitoa tamko la kuruhusu idadi ndogo ya mashabiki wa soka kuweza kuingia kwenye viwanja vya timu kadhaa zilizoruhusiwa.

Hii inakuja baada ya serikali ya nchi hiyo kusitisha uwepo wa mashabiki viwanjani toka mwezi Machi kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19.

Licha ya kwamba tamko la kuruhusu uwepo wa mashabiki limeonekana kama litawanuafaisha wachache na kukandamiza wengine. Kocha wa Liverpool – Jurgen Klopp anaamini huo ni ueleko sahihi kwa kipindi hiki kigumu kwa kila mtu.

Jurgen Klopp anasema “sote tunasubiri hatua ndogondogo kama hizi katika uelekeo sahihi, sio kwenye soka tu bali kwenye kila sehemu ya maisha.

“Kugawa kanda ni wazo zuri kwa sasa nchini, kwahiyo itategemea na idadi ya watu walioathirika kwa muda husika.

“Ninaelewa majadiliano ya namna ilivyofaida kwa baadhi ya timu – lakini suala sio faida bali ni hatua sahihi.

“Hii ni ishara njema – ninafurahi tunaweza kuruhusu watu 2,000. Hakuna mtu anayejua itakuwa kwa muda gani, lakini ninadhani tusilijadili hili kwa kuangalia faida na hasara kwenye timu. Ni hatua kwenye uelekeo sahihi.”

Brighton Albion, Everton, Liverpool, Southampton, Arsenal, Chelsea, Tottenham, West Ham United, Crystal Palace na Fulham ndio timu pekee zitakazoweza kuwa na mashabiki 2,000 viwanjani kwenye michezo yao ya nyumbani.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa