Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp wakati anaongea na waandishi wa habari amesema kuwa kikosi chake kina hali nzuri na sana japo kuna uwezekano wa wachezaji wawili wasicheze kwenye kikosi licha ya kusafiri na timu.

Fabinho na Thiago walikuwa wanasumbuliwa na mejeruhi, huku Fabinho akikosa michezo mitatu iliyopita, Pia Thiago kuna wasiwasi kwa kutokucheza kwenye mchezo wa fainali kutokana na kupata majeraha kwenye mchezo wake wa mwisho.

Ila wote wamesafiri na timu na tayari wameshatua jijini Paris siku ya ijumaa na Jurgen Klopp amethibitisha hilo pindi tu alipotua kwamba wachezaji hao wawili bado wapo kwenye majadiliano kama itawezekana kucheza mchezo wa fanali.

“Tuna hali nzuri, nzuri sana. Tuna furaha ya kuwa hapa.” Jurgen Klopp alisema kwenye kikao na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa fainali ya kesho.

“Inaonekana wanaendelea vizuri kwa wote. Fabinho amefanya mazoezi kawaida, Thiago amefanya mazoezi jana na leo kwaiyo tunaweza kuandelea kuanzia hapo.”

Jurgen Klopp alipoulizwa kuhusu nani anampa nafasi kwa kesho alijibu: “Sijui, sina jipu rahisi. Kama utaangalia historia ya klabu na jinsi Real Madrid wanavyosherekea  wanavyofanikiwa kurudi wakiwa wamepoteza basi nitakwambi wao ni wazoefu.

“Nataka sisi tuwe kwenye uwiano sawa na aina hiyo. Nataka tuwe sisi kwa mchezo mzima, ikwa tutautawala mchezo wetu tutakuwa wagumu kucheza.

“Jambo muhimu kwetu ni kuwa sisi na kujiamini, sijui nani ananafasi zaidi na sijari kabisa.”


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa