Juve na Ac Millan Nusu Fainali iliyo Akisi Picha ya Fainali

Licha ya yota wa Juventus na timu ya taifa ya ureno Christiano Ronaldo kukosa penati kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la italia lakini timu hiyo ya Juventus imefanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa faida ya goli la ugenini, ambapo kwenye mchezo wa awali walienda sare ya kufungana goli 1-1 wakati mchezo wa hapo jana walipata sare nyingine ya kutofungana.

Kwenye mchezo wa awali Juventus walianza kupata goli kunako dakika ya 13 ya mchezo baada ya kupata penati ambayo ilipigwa na Christiano Ronaldo, lakini baadae Ac milan walipata bao la kusawazisha hivyo kufanaya dakika tisini zimalizike kwa kutunishiana misuli kwa kutoka 1-1.

Kwenye mchezo huo wa marudiano AC milan iliwakosa nyota wake kama  Zlatan Ibramovic kufuatia kuwa na majeraha huku Samu Castillejo na Theo Hernandez waliukosa mchezo huo

Mechi ya marudiano ilipigwa siku ya ijumaa juni 13 walienda sare nyingine ya kutofungana goli hivyo Juventus kufanikiwa kwenda hatua ya fainali kwa faida ya goli la ugenini, na kuwa fanya Juventus kuongeza rekodi ya kutinga fainali kwa mara ya 19, huku timu ya As Roma kuwa ni ya pili kwa rekodi hiyo kwa kufika fainali ya kombe hilo la Italia  mara 16

Fainali ya kombe la italia itafanyika tarehe 17 juni ikiwakutanisha kati mshindi atakae patikana kati ya Napoli dhidi  Inter milan  na timu ya  Juventus , lakini  pia Juventus siku ya juma tatu watacheza   mechi yao dhidi ya Bologna wakiwa ugenini kwenye ligi ya serie A

Siku ya mchezo huo Juventus na Ac milan heshima zao kwa wafanyakazi wote waliojiweka mstari wa mbele kukabaliana na maambukizi ya virusi vya korona  na wote waliopoteza maisha tangu  kuzuka kwa virusi hivyo hatari

39 Komentara

    Dah, mnyama Cr7 sio wa kukosa tuta kabisa, ila sio mbaya fainali kitaeleweka tu

    Jibu

    Mtanange wakufa mtu huo patakuwa apatoshi

    Jibu

    Dah ilikuwah bonge la game yan nilitaman mpra usingekwisha

    Jibu

    Miaka ya karibuni AC Milan sio ile ya akina Ronaldo De Lima , Gattuso na wengineo. Wamechoka hawana uwezo kuingia sokoni na kutafuta wachezaji wa watakaorejesha heshima iliyopotea. Hata hivyo walijitahidi#meridianbettz

    Jibu

    Kwa Sasa imebaki story tu hakuna ushindani kama wa kipindi like cha akina dilima saivi Milani imebaki jina tu

    Jibu

    Tunasubiri kwa hamu sana mana itakuwa cr7 anahasira ya kukosa penat hivyo atawaumiza watu jamani

    Jibu

    Jaman. Hii sijui itakuaje

    Jibu

    Ac millan sio powa hatoniangusha

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    dah hii mechi nimeikosa

    Jibu

    Patakuwa hapatoshi

    Jibu

    Juve atakomba makombe yote ya Italy, lakini UEFA haiwezi kamwe

    Jibu

    Hii mechi ilikuwa kali sana

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Sipatiii picha itakavyokuwa siku hiyo

    Jibu

    Mechi Kali Sana hiyo.

    Jibu

    Fainali itakuwa bora zaidi

    Jibu

    bila ya kupepesa macho jibu lipo wazi juve bila jasho mechi wa shinda hiyo

    Jibu

    Mechi iko vizur sana

    Jibu

    Nilijua tuu kuwa mechi hii wababe tupu

    Jibu

    Duuuh ilikuwa bonge la mechi

    Jibu

    Juve watachukua tu #Meridianbettz

    Jibu

    Juve mabingwa lazima wachukue ubingwa#meridianbettz

    Jibu

    Mpira ni dakika 90 tunasubiria kuona mshindi

    Jibu

    Juventus wataibuka na ushindi

    Jibu

    Juve alikuwa na kila sababu ya kushinda hii game alikosa bahati tu

    Jibu

    Mpira dakika 90 tutampata mshindi#meridianbettz

    Jibu

    Ilikuwa bonge la mechi yenye kandanda safi sema tu Milan hakuwa na Bahati

    Jibu

    ngoje tuone iyo siku nani ataibuka mshindi

    Jibu

    Juve walistahili kuingia fainal#meridianbettz

    Jibu

    Lilikuwa bonge la mechi

    Jibu

    Juve wakaze buti wachukue ubingwa

    Jibu

    Ac milan wako vizuri.

    Jibu

    Mtanange sio powa tusubili matokeo

    Jibu

    Juventus lazima wachukue ubingwa#meridianbettz

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Juve wapo vizuri ubingwa ni lazima

    Jibu

    Tunasubilia kwa hamu mpaka kieleweke

    Jibu

    Good

    Jibu

Acha ujumbe