Ni ule wakati wa kuzitazama sajili mbalimbali barani Ulaya na hata hapa kwetu Tanzania. Juve kuingia mazungumzoni na wawakilishi wa Paul Pogba.
Wakati hapa nchini kukiwa na taarifa mbalimbali miongoni mwa mashabiki wa Simba SC kuhusu Bernard Morrison, Ulaya napo kuna Paul Pogba. Hawa jamaa wanafanana kwa tabia zao, tofauti ni geografia walizopo tu.
Taarifa rasmi kutoka Simba ilisema Morrison ameachwa na timu hiyo kwa sababu za kifamilia na kwamba, hatokuwa sehemu ya timu hiyo kwa michezo iliyosalia msimu huu. Taarifa hii inapelekea mashabiki kuamini kuwa, Simba wametupa jiwe gizani. Hii inamaana kuwa, wamemtema Morrison kimyakimya.
Pogba naye anayake, dakika 6 za mwanzo kwenye mchezo dhidi ya Liverpool zilimtosha kucheza mchezo wa mwisho akiwa na jezi ya Man United. Aliumia mguu na, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia msimu huu.
Pamoja na yote, Juve wanaripotiwa kuingia mazungumzoni na wawakilishi wa Paul wakijaribu kuangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo kule Turin. Kama itawezekana, hii itakua ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kujiunga na Juventus kama mchezaji huru akitokea Manchester United.
Pamoja na Juve, inasemekana PSG walishafanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo na kwamba, Pogba anachokifanya sasa hivi ni kuangalia upepo upi aufuate baada ya msimu huu kumalizika.
Kwa upande wa Morrison kunafununu kwamba wananchi kule Jangwani (Yanga) wanataka kumrudisha. Ndio kwamba nyumbani kumenoga? Macho na maskio yapo sokoni kwa wapenda soka!
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.