Juventus Kulipa £62.8Milioni kwa Dusan Vlahovic

Klabu ya Juventus wamekubaliana na klabu ya Fiorentina kumnunua mshambulliaji wao Dusan Vlahovic kwa ada ya uhanisho wa kiasi cha £62.8Milioni kwenye dirisha hili January.

Klabu ya Juventus na Fiorentina wamekuwa wakifanya majadiliano kwa muda mrefu, kuhusu ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo wa kimataifa kutokea Serbia kuhusu ada ya uhamisho wake kwa muda sasa.

Juventus
Juventus

Fiorentina walikuwa na mpango wa kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 21 dirisha hili, ili kuweza kuongeza faida baada ya kubakisha miezi 18 kwenye mkataba wake, huku vilabu za Uingereza ambavyo ni Arsenal na Tottenham nazo zilikuwa zinawania saini ya mshambuliaji huyo.

Mkurugenzi wa klabu ya Fiorentina Daniele Prade aliiambia Sportitalia: “ni thamani nzuri zaidi ya €70milioni pasipo makubaliano ya ubadilshanaji wa mchezaji yeyote na hakuna malipo yoyote ambayo yatakuwa upande wetu.

Juventus

“Milango yote iko wazi kwenye swala hili, kwa sababu tunahitaji kuelewa ni nini mchezaji na wakala wake wanataka kufanya, tuko tayari kwa mazungumzo na tumeshatoa offa mbalimbali kwa ajiri ya kumuongezea mkataba, na pia kuna offa ya kumuuza ina ushawishi mkubwa.

“Nasema hivi kwa sababu klabu yetu inatengeneza faida ya €75milion kwa mwaka na hatuwezi kuipoteza rasilimali muhimu bure bure tu.”

Vlahovic amekuwa na msimu mzuri tokea msimu uliosha ambapo aliweza kufunga magoli 21 kwenye michezo 40 kwa klabu yake pia msimu huu ameweza kuendelza makali yake baada ya kufunga magoli 20 kwenye michezo 24 kwenye mashindano yote mpaka sasa.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe