Klabu ya Juventus inajiandaa kurumdisha kiungo nyota wa klabu ya Man Utd Paul Pogba kwa mara ya pili tena baada ya kumsajiri mwaka 2012 kama mchezaji huru na wanatarajia tena kumsajiri kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu.
Juventus ni moja ya chaguo lilipo kwenye meza ya Paul Pogba ambapo bado anamarafiki wengi kwenye viunga vya Turin, lakini hataweza kuungana na rafiki yake wa karibu Paulo Dybala, ambaye ataondoka baada ya mkataba wake kuisha na miamba hiyo ya Italia.
“Huu mwaka, Umekwisha, hatutashinda kombe lolote, kama nikiwa na Manchester au klabu nyingine, nataka kushinda makombe,” aliliambia Le Figaro wiki iliyopita.
Kulingana na taarifa za klabu ya Juventus, haiwezi kulipa zaidia ya €10milioni kama mshahara wa mchezaji huyo mwenye miaka 29. Dybala chanzo cha kuondoka kwenye klabu hiyo ni tatizo la kimshahara.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.