Mlinzi wa Juventus Merih Demiral hatakuwepo dimbani kwa siku zisizopungua 10 baada ya kupata tena jeraha.

Demir, ambaye ni nyota wa kimataifa wa Uturuki aliondolewa dakika 69 kwenye ushindi wa 3-0 Jumatano dhidi ya Dynamo Kiev katika Ligi ya Mabingwa.

Nyota huyu alikuwa anarejea kwenye kikosi cha kwanza cha Juve baada ya kukosa michezo miwili kutokana na jeraha dogo alilolipata kwenye mechi dhidi ya Cagliari Novemba 21.

Miamba ya Italia ilithibitisha rasmi kupitia tovuti yao Salamis hii kwamba Demiral amepata Jeraha kwenye paja la kulia.

Juventus Demiral

Nyota huyu wa miaka 22 ataikosa debi ya Serie A wikendi hii dhidi ya Torino, na pia safari ya wiki ijayo ya Ligi ya Mabingwa dhidi Barcelona.

Juventus, ambao sasa wapo nafasi ya nne katika msimamo wa Serie A baada ya mechi tisa, pia wana michezo dhidi ya Genoa, Atalanta, Parma na Fiorentina katika kuelekea kuumaliza mwaka.

Demir amekua akitumika na kocha mkuu Andrea Pirlo mara tisa katika mashindano yote msimu huu, akiwa ameanza katika mechi tano kwenye Serie A.


 

URAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Juventus, Juventus Kumpoteza Merih Demiral Siku 10, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

18 MAONI

  1. Nyota huyu alikuwa anarejea kwenye kikosi cha kwanza cha Juve baada ya kukosa michezo miwili kutokana na jeraha dogo alilolipata

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa