Klabu ya Juventus ilikuwa imepanga kumfanyia sherehe mshambuliaji wake Paul Dyabala ya kumsainisha mkataba mpya kabla ya maongezi kuvunjika na kuamua kumuacha aondoke huru kwenye majira ya kiangazi baada ya msimu kuisha.
Jana wakala wa Dyabala alieleza kuwa hivi karibuni walifanya kikao na klabu ya Juventus ambacho kilikuwa cha mwisho, baada ya kushindwa kukubaliana vipengere vipya kwenye mkataba mpya, klabu imeamua kuachana na mpango wa kumpa mkataba tena.
Kulingana na gazeti la “La Stampa” linadai kuwa klabu ya Juventus, ilianda sherehe ya kusherekea kufanikiwa kwa kumuongezea mktaba mpya mshabulliaji wao Paul, kabla mambo kwenda mrama na kusitisha, huku wakifungia zawadi zote ambazo ziliandaliwa kwa ajiri yake.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Argentina, anatarajia kuondoka kwenye klabu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha mwezi June.
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.