Taarifa kutoka vyanzo vya habari za kimichezo nchini Italia zilibainisha kuwa klabu ya Juventus inataka kuwacheleweshea mishahara wachezaji wake, na tayari ilikuwa imeshawaomba wachezaji kukubaliana na suala hilo.

Suala hili liliripotiwa mapema mwezi Aprili pia ba chapisho la Il Corriere dello Sport, ambao walibainisha kuwa Juventus walikuwa wanapanga kuwacheleweshea wachezaji mishahara, na walikuwa kwenye mchakato wa kufanya makubaliano hayo na wachezaji wakihusisha mishahara ya Machi, Aprili na Juni.

Juventus: Pirlo Akanusha Kuchelewesha Mishahara

Mwakajana, wachezaji walikubali kucheleweshewa mishahara baada ya changamoto ya Covid 19. Hii iliwasaidia Juventus kuwa na akiba ya takribani €90m, lakini mwaka huu suala hili bado lipo mikononi mwa wachezaji kuamua kama watakubaliana na kucheleweshwa kwa malipo.

Hata hivyo, kabla ya mechi dhidi ya Sassuolo wiki hii, meneja Andrea Pirlo aliulizwa juu ya suala hili na ikiwa tayari wachezaji wameomba kukubaliana na kucheleweshewa malipo. Pirlo amepinga kuwa hakuna suala hilo kwa sasa mambo yako sawa kama kawaida.

“Hapana, kwa sasa, kila kitu kipo sawa. Hatujasikia chochote juu ya hili, na malipo wakati wote yamekuwa yakija kwa wakati na tuna amani” 

– Andrea Pirlo


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Juventus, Juventus: Pirlo Akanusha Kuchelewesha Mishahara, Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa