Kwa mujibu wa Tuttorsport, Zinedine Zidane na Gennaro Gattuso ndiyo mameneja wanaotazamwa kwa ukaribu zaidi kuichukua nafasi ya Andrea Pirlo mwisho wa msimu.

Meneja wa sasa, Andrea Pirlo anatarajiwa kutimuliwa bila kujali nafasi ya Juventus itamaliza nafasi ya ngapi  kwenye Serie A.

Juventus hawawezi kuvumilia kukosa kumaliza nne bora, lakini kupata nafasi ya Ligi ya Mabingwa sio sharti pekee la kwa Maestro klabuni hapo.

Kwa mujibu wa Tuttosport, Zinedine Zidane na Gennaro Gattuso wameibuka na kupigiwa chapuo zaidi kuchukua nafasi ya Pirlo mwishoni mwa msimu.

Zidane ni mlengwa wa muda mrefu wa Andrea Agnelli, ambaye alitaka kumuajiri 2019, kabla ya kocha huyo Mfaransa kukubali kurejea Real Madrid.

Hata hivyo, mshahara wa Zidane wa euro milioni 12 kwa mwaka ni kikwazo katika uwezekano wake wa kurudi Turin kwani Juventus yuko katikia mchakato wa kupunguza gharama kutokana na janga la COVID.

Gattuso, ambaye anatarajiwa kuondoka Napoli mwishoni mwa msimu, anaweza kuwa kocha mwenye bei nafuu zaidi.

Wakala wake Jorge Mendes ana uhusiano mzuri na watendaji wa Juventus, maelezo ambayo yanaweza kuwezesha mpango unaowezekana.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Gattuso, Juventus: Tumchukue Gattuso au Zidane?, Meridianbet

SOMA ZAIDI

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa