Mfumo wa kutumia wachezaji wa zamani kama makocha wa timu husika haujaanza jana wala leo ila kwa sasa imekuwa dili kubwa kwa vilabu duniani kote.

Manchester United walimkabithi nafasi ya ukocha Ole Gunnar mchezaji aliyewapa makombe mengi Manchester United miaka ya 90.

Chelsea wamemkabidhi timu frank Lampard kuinoa na ikumbukwe mchezaji huyo wa zamani aliitumia asilimia 90 ya maisha yake ya soka kuitumikia Chelsea.

 

Juventus Wafwata Nyayo za Madrid,United.

 

Mikel Arteta aliwahi kuichezea timu ya Arsenal enzi za Arsene Wenger na sasa anainoa timu hiyo huku akiwa na historia ya kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa FA.

Zinedine Zidane amekua akiifundisha Real Madrid kwa miaka mitano sasa huku akiipa timu hiyo ubingwa wa ulaya mara tatu mfululizo. Ikumbukwe Zidane aliituumikia vyema Real Madrid kama mchezaji na kuwapa makombe mbalimbali.

 

Juventus Wafwata Nyayo za Madrid,United.

Klabu ya Juventus imemfuta kazi kocha wake Mario Sarri na kumkabidhi aliyekuwa mchezaji wao wa zamani Andrea Pirlo.

Juventus wamefanya maamuzi ya kumfuta sarri baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora tena na timu kama Lyon.

Andrea Pirlo alikuwa mchezaji wa Juventus kuanzia mwaka 2011 hadi 2015 akicheza michezo 119 na kufunga mabao 16.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

42 MAONI

  1. Mimi nafikiri juve wamefanya kitu kizuri au laah mana kazi ya ukocha sio mchezo na ninaamini kama wamemteuwa kuwa Andrea Pirlo ndiye kocha basis Mimi kama shabiki nasubiri kuona mambo mazuri

  2. Ni kweli imekua kama jadi clabu yingu zimekua zikiwatumia wachezaji wazamani kua makocha tumeona vilabu vingi wakifanya hivyo sasa wakati wa juve kumkabizi timu Andrea pirlo

  3. Hii inapendeza sana kwa sabab kocha aliechezea club anayo fundisha anakua na ule uzalendo tofauti ukimleta morinho au kocha mwengine anakua hana uchungu na club anayo fundisha

  4. Nadhani club nyingi zimekuwa zikitambua mchango wa wachezaji wao wa zamani hivyo wanaamini kuwa ni chaguo sahihi sababu wanajuwa Falsafa za timu husika

  5. Inapendeza kwenye ulimwengu wa soka la miguu kuongezeka idadi ya makocha wachezaji waliotoka club walizokua wakizichea katika career yao ya soka la miguu.

  6. Juventus wamefanya maamuzi ya kumfuta sarri baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora tena na timu kama Lyon.

  7. Ndo ulimwengu wa sasa kila club inatengenezah nafas kwa malegendary wao kuwa ma meneja kwny timu zao au nafas yyte ya juu katika club husika walizochezah

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa