Juventus wamepiga hatua kubwa kwenye dirisha la usajili, wakipata mwanga wa awali kutoka kwa mshambuliaji wa Manchester United Joshua Zirkzee kujiunga nao. Nyota huyo wa Uholanzi, mwenye umri wa miaka 25, anataka kurejea Italia baada ya kipindi kigumu England.

Kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, mazungumzo yanaendelea kupitia wakala wake Kia Joorabchian, huku Juve wakitaka kufanikisha dili la mkopo. Wakati huohuo, uongozi wa Turin unafanya kazi ya kukamilisha usajili wa Randal Kolo Muani kutoka Paris Saint-Germain kwa takriban €40m, ili kuunda safu mpya ya ushambuliaji kwa kocha Luciano Spalletti.
Zirkzee akiwa Bologna msimu wa 2023-24 alifunga mabao 12 na kutoa asisti 7. Ameshindwa kupata nafasi ya kudumu United, akianza mechi 19 pekee kati ya 68 za ligi kwa misimu miwili. Ana sifa za kiufundi na uwezo wa kushiriki kwenye mfumo wa pressing wa Spalletti.

Vilevile, kumekua na uhitaji wake wa muda mrefu kutoka kwa mkurugenzi mpya wa soka Ricky Massara, aliyewahi kumtaka akiwa Roma. Juventus wanahitaji haraka washambuliaji wapya baada ya jeraha la mchezaji Jeff Ekhator.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Wanataka kuchanganya ubora wa kiufundi wa Zirkzee na kasi ya Kolo Muani ili kuunda safu ya ushambuliaji yenye nguvu na ushindani zaidi. Kocha Spalletti anasubiri uongozi kuthibitisha muda wa kukamilisha dili hizi kabla ya maandalizi ya msimu.

Juventus wanakabiliwa na mtihani wa mapema Serie A, wakianza na mechi ya ugenini dhidi ya Frosinone tarehe 23 Agosti. Hivyo, kukamilisha usajili wa Zirkzee na Kolo Muani mapema ni muhimu ili wazoee mfumo wa timu kabla ya msimu kuanza.


