Christian Pulisic anawindwa na klabu ya Juventus ya huko nchini Italia ambapo timu hiyo ipo  kwenye rada zao huku kukiwa na sintofahamu juu ya mustakabali wa Mmarekani huyo nchini Uingereza. Mchezaji huyo mpaka sasa  ana umri wa miaka 24.

 

Juventus Yamuwinda Pulisic

Christian Pulisic amekuwa nadra sana kuonekana kwa klabu hiyo ya London Magharibi msimu huu, akiwa amecheza kwa dakika 156 pekee kwenye ligi ya Primia. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Marekani alihusishwa na kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto, wakati United wakiripotiwa kutaka kumchukua kwa mkopo.

Kulingana na Tuttosport, Juventus wanafuatilia kwa karibu hali ya Pulisic huku wakiangalia uboreshaji wao wa safu ya mbele, huku mkataba wake ukiisha 2024 kwahiyo anaweza kuwa sokoni kwa ada iliyopunguzwa iwapo ataamua kuachana na Potter. Juventus mpaka sasa ipo chini ya Allegri.

Katika msimu wa 2019/20, mchezaji huyo wa Kimataifa kwenye mechi 51 alichangia mabao 13 katika kampeni ambayo iliifanya Chelsea kumaliza katika nafasi ya nne kwenye ligi ya Primia, lakini tangu wakati huo imekuwa ngumu kufikia viwango hivyo.

 

Juventus Yamuwinda Pulisic

Mchezaji huyo wa zamani wa Borrusia Dortmund alikiri kwamba alikuwa na uhusiano mbaya na kocha mkuu wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel na alikatishwa tamaa zaidi na ahadi ambazo hazikutimizwa. Alisema Pulisic kuwa;

“Nilifikiri kwamba nimepata mwanzo, na muhimu zaidi alikuwa amenihakikishia hapo awali kwamba ningeanza”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa