Licha ya kwamba kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara mtupiaji namba moja ni Prince Dube wa Azam FC, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa nyota wake Kagere atamaliza akiwa ni namba moja.
Kagere ni mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo, aliibuka mfungaji bora msimu wa 2018/19 akiwa na mabao 23 na msimu wa 2019/20 akiwa na mabao 22.
Msimu huu wa 2020/21 amekutana na chuma, Dube ambaye anampa presha akiwa ni mtaalamu wa kucheka na nyavu ndani ya Azam FC, ametupia mabao 12.

Kagere yeye msimu huu mpaka sasa ametupia jumla ya mabao 11 na mshikaji wake John Bocco ana mabao 10 ndani ya Ligi.
Gomes amesema:“Ninawaamini wachezaji wangu hasa katika safu ya ushambuliaji imani yangu ni kwamba watamaliza wakiwa juu katika suala la ufungaji hilo sina mashaka nalo.
“Suala la muda na utulivu kwao litawafanya wafikie malengo yao ipo wazi ushindani mkubwa nao wanashindana pia,”.
Kwa sasa Simba ipo Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs ambao ni robo fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, unatarajiwa kuchezwa Mei 15.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
msimu huu MK 14 amekuwa akicheza dakika chache mno ndio hana idadi kubwa ya magoli labda atapewa nafasi zaidi msimu ujao
Kijana anakubalika na mashabiki
Mm na namkubali sana kagere
Kagere yupo vizuri
Vizuri sana
Kagere namkubali sana
Sifa ziende kwa kagere
Kijana anakubalika na mashabiki
Jamaa jembe
Kagere yupo vizuri
Duuuh sawa
Apewe nafax zaid
Hana maajabu
Apambane tu ndo la msingi.
Yupo vizuri
Jamaal yupo vzr
Yupo vizur
Kagere jembe