STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa usajili ambao umefanywa na klabu hiyo ni mzuri na unaweza kuisaidia timu kufanya vizuri msimu ujao kwenye mashindano ingawa usajili ni kam kamali.

Meddie alisema kuwa, mambo yanaweza kubadilika licha ya kusajili wachezaji bora kwa sababu mpira una mambo mengi na lolote linaloweza kutokea kinyume na matarajio ya watu wengi.

 

kagere, Kagere Aufungukia Usajili Mpya Simba., Meridianbet

Akizungumzia usajili huo wa Simba Meddie alisema: “Usajili ni mzuri lakini siwezi kuzungumzia sana hilo kwa sababu mpira una changamoto zake unaweza ukasajili majina makubwa kwenye timu na ukashindwa kufanikiwa.

 

“Unaweza ukamleta, Messi na Ronaldo na ukashindwa kufaya vizuri. Nafikiri hilo ndiyo neno pekee ambalo naweza nikazungumza juu ya usajii.”

Kagere ameungana na wachezaji wengine wa Simba kwenye maandalizi ya msimu mpya katika kambi ambayo imwekwa kwenye mji wa Ismailia nchini Misri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa