Inaelezwa kuwa mshambuliaji namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck haziivi chungu kimoja jambo linalomfanya ajenge ushkaji na benchi.

Kagere, Kagere Huenda Akaondoka Simba, Meridianbet

Hali hiyo inatajwa kuwa sababu ya Kagere kuwaza kusepa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa hajui hatma yake itakuaje kwenye maisha yake ya kucheza ndani ya uwanja.

Kagere amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu ambapo inaelezwa kuwa alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma ila aliitwa kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda.

Kagere, Kagere Huenda Akaondoka Simba, Meridianbet

Kwa msimu huu wa 2020/21 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikiwa imecheza mechi mbili na kutumia dakika 180 uwanjani, nyota huyo ametumia dakika mbili pekee.

Wakati ikishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau Uwanja wa New Jos, Kagere aliishia benchi huku mchezo wa pili Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikiambulia sare ya bila kufungana aliingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya John Bocco na kutumia dakika mbili ndani ya uwanja.

Kagere, Kagere Huenda Akaondoka Simba, Meridianbet

Suala hilo linatajwa kuwa sababu ya chanzo cha nyota huyo kufungua njia ya kusepa ndani ya kikosi hicho ambacho amekifungia jumla ya mabao 49 ndani ya ligi.

Vandenbroeck amesema kuwa wachezaji wake wote wana uwezo mkubwa wa kucheza na kila mmoja ana umuhimu wake.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

Kagere, Kagere Huenda Akaondoka Simba, Meridianbet

SOMA ZAIDI

18 MAONI

  1. Simba washaona wepata mchezaji mwingine bora zaidi yako ndio mana hasaivi wanakuweka benchi jiongeze baba timu zipo nyingi zinazotaka wachezaji kama wewe

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa