Kahata na Simba

Huku upande wa pili ukiendelea kufanya usajili kwa vurugu, mabingwa wa ligi msimu huu, klabu ya Simba wao wapo kimya kabisa bila kelele wala kitisho chochote kutokana na usajili unaofanywa na majirani zao. Kwao hilo jambo haliwatishi wala kuwapa nafasi ya kuwaogopa kwa kile wanachokifanya ya kwamba hakina athari kwao.

Kwa malengo ya klabu wao hawasajili kila eneo ila wana maeneo yao maalum ambayo wanaona kabisa yanahitaji marekebisho kwa kiasi fulani ili kuwaweka kwenye hali ya ushindani zaidi, jambo ambalo kama kikosi ambacho kimewekeza kwenye soka wanaliangalia na namna wanavyoweza kunufaika na mchezaji huyo.

Mbali na hayo, klabu hiyo imejaribu kupeleka taarifa za awali kama wataweza kumnasa mchezaji huyo ambaye ndani ya Gor Mahia amekuwa mhimili mkubwa sana. Kiungo huyo anatazamiwa kuja kuongeza radha ya soka hasa eneo la katikati ambapo timu nyingi miaka ya sasa zinaangalia mifumo inayozingatia sana uhai wa eneo la kati.

Mara nyingi timu zenye kikosi chenye uimara na muunganiko eneo la katikati basi lazima mabadiliko yaweze kufanyika ili kukipa nguvu kikosi husika. Jambo pekee ni kwamba kukiwa na timu inayomuogopa nyota fulani mara kadhaa huwa na utata kutokana na yule anayesajiliwa kuwa na uwezo ambao unakuwa tishio upande wa pili.

Kiungo huyo hatari amethibitisha kwamba miamba hao wa soka Tanzania tayari wameonesha nia ya kumsajili ndani ya kikosi chao ili aweze kuongeza nguvu zaidi; hicho ni aina ya kikosi cha kiushindani ambacho Simba wanakiandaa na kwa hakika kitaweza kuwafaa kabisa kutokana na mfumo wao wanaoutumia kwa sasa.

Anafaa kwa nafasi yoyote ile atakayopewa kuicheza kutokana na uwezo wake na kiwango alichonacho na alichokionesha kwa siku za karibuni alipokuwa akitumikia mechi zake na klabu yake ya sasa; pia mechi zake za kimataifa amekuwa sehemu ya mchango mkubwa sana na anastahili kukutana na mabingwa hao wa ligi Tanzania.

Hana kinachomzuia kutua Simba kwa sababu mkataba wake ndani ya klabu hiyo ya Kenya umefika ukomo na kwa sasa yupo huru kabisa kuchagua kwa kwenda katika maisha yake ya soka, endapo ataendelea kusalia Kenya au kuangalia zaidi sehemu nyingine kwenye soka la ushindani hiyo ndiyo nafasi yake kwa sasa.

Kutokana na taarifa hiyo bado hajatoa ripoti yoyote japo anategemewa kuzungumzia chochote mara baada ya kumalizika kwa michezo ya mataifa ya Afrika kule Afrika kusini. Huo ndiyo wakati wake yeye kusema chochote kuhusu mstakabali wake katika soka kwa msimu ujao. Wanasema siku zote kizuri hujiuza.

3 Komentara

    Yupo vizur

    Jibu

    Anajua

    Jibu

    Fundiii kutoka nairobeeeh mwamba sana

    Jibu

Acha ujumbe