Kahn: Kiwango cha Gnabry, Flick Anahusika.

Gwiji wa Bayern Munich – Oliver Kahn amesifu kiwango cha Serge Gnabry baada ya kung’ara kwenye Mashindando ya Ligi ya Mabingwa – UEFA msimu huu.

Gnabry ambaye mpaka sasa anajumla ya magoli 9, amekuwa kwenye kiwango thabiti msimu huu akicheza katika nafasi ya winga. Katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Lyon, Gnabry alifunga magoli mawili kati ya matatu yaliwapeleka Bayern hatua ya fainali na sasa, Bayern Munich atamenyana na PSG.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kahn amesema ” magoli yake ni ya kiwango cha dunia. Ni mchezaji aliyeongezeka kiwango kwa miezi kadhaa iliyopita. Grafu yake inapanda kila mwaka. Yupo mbali kufikia kiwango cha dunia lakini ni mchezaji mzuri, anamchezo mzuri.

kahn
Gnabry akipongezwa na kocha wake Hansi Flick

“Lakini pia kocha anahusika, mawasiliano ya kocha. Hiyo ni sifa mojawapo ya Hansi [Flick]. Anaweza kushughulika na wachezaji wa aina mbalimbali, mara zote ana maneno sahihi ya kuzungumza. Hiyo inatuletea mafaniko kwa sasa.

Kahn awapongeza pia wachezaji wenye uzoefu.

“Nimelinganisha vitu vingi sana kwa uzoefu wangu. Kwa namna ambavyo hawa wachezaji wanawaza magoli, ni jambo la kuvutia. Wanataka kushinda Ligi ya Mabingwa,watafanya lolote kwa ajili hiyo lakini unatakiwa kuwa na muongozo.

“Tunae Manuel Neuer kama nahodha anayeweza kuwaongoza wachezaji wengine. Thomas Muller pia amekuwa mfano wa kuigwa na wengine, anazungumza sana. Joshua Kimmich anamorali sana, anafanya kila kitu kwaajili ya maendeleo.

“Kitu cha kipekee ni kwamba, wengi wao wameshashinda kila kitu lakini bado hawachoki.”

Bayern Munich hawajapoteza mchezo wowote 2020 wakiwa tayari wamecheza michezo 20. Ushindi dhidi ya PSG utakamilisha jumla ya mataji 3 kwa Bayern Munich msimu huu.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi Ucheze

36 Komentara

    Gnabry anakiwango kizuri sana hata hivo safu ya ushambuliaji Bayern imejitosheleza wapo vizuri sana

    Jibu

    Habari njema Sana

    Jibu

    Flick ni kocha mzur na kaul ambayo alioongea kahn yuko sahihi kabisa

    Jibu

    Gnarby amekuwah mcharo kwl mmoja wa wachezaj walionyesha kiwango cha Hal ya juu ue

    Jibu

    Ni kwer kwasasa uwez wake unaongezek

    Jibu

    Kijana yuko Fiti

    Jibu

    Jamaa Yuko vizur

    Jibu

    Yupo kiwango

    Jibu

    Kitu cha kipekee ni kwamba, wengi wao wameshashinda kila kitu lakini bado hawachoki.”

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Jamaa Yuko vizuri

    Jibu

    Yuko vizur sana!

    Jibu

    Kusema ukweli kocha anastahili pongezi zake kwa kumfanya Gnabry Ang’ae sana si tuu ndani ya UEFA bali ata kwenye ligi

    Jibu

    Ni kweli kabisa Flick amehusika sana#Meridianbettz

    Jibu

    Gnabry yupo vizuri sana

    Jibu

    Yuko vzuri

    Jibu

    Good job koch

    Jibu

    Maoni:vizuri sana inabidii aongezee juhudi sasa

    Jibu

    Gnabry yupo vizuri kiwango chake cha kimataifa hasa kwenye safu ya ushambuliaji

    Jibu

    Ni kweli kwa sasa uwezo wake umeongezeka#Meridianbettz

    Jibu

    Good job koch#meridianbettz

    Jibu

    ni kweli kwa sasa hivi kiwango change kimeongezeka

    Jibu

    Habari njema Sana
    @meridianbettz

    Jibu

    kocha yuko vizuri sana kazi ameifanya ya ziada

    Jibu

    Kiukweli bado Bayern munch wana kikosi kizuri na ndio mabingwa wetu msimu hii asilimia mia PSG wajipange sana hawana mbio za kuwafikia bayrne hata waluke

    Jibu

    Kijana yupo vizuri kwa Sasa kiwango chake kimezidi kuwa juu

    Jibu

    Gnarby ni mchezaji anayejituma sana lazima kiwangi chake kipande

    Jibu

    Ameng’aa sana kipindi kifupi kuanzia kwenye uefa hadi ligi

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

    Namkubal

    Jibu

    Namkubali.

    Jibu

    Munich msimu wenu huu

    Jibu

    Kweli maisha yanabadilika arsenal walimuona Kama sio msaada kwao sasa dogo amekua gumzo ulimwenguni.

    Jibu

    Kijana yuko fit na amekua kwenye kiwango kizr sana

    Jibu

    Ni sahihi jamaa kiwango chake kimekngezeka

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.