Kiungo wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Kalvin Phillips anafikiria kutimka ndani ya klabu hiyo katika majira ya baridi ya mwezi Januari.

Kiungo Kalvin Phillips inaelezwa anafikiria kuondoka ndani ya klabu hiyo kwajili ya kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kitu ambacho hajakipata ndani ya kikosi cha Man City mpaka sasa.kalvin PhillipsKiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye alijiunga na Manchester City mwaka 2022 akitokea klabu ya Leeds United amekua hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya klabu hiyo na sababu kubwa ikiwa ni majeraha ambayo amekua akiyapata.

Manchester City na kiungo huyo inaelezwa wamekaa chini na wote wamekubaliana kuachana katika dirisha dogo la mwezi Januari, Kwani mchezaji huyo anataka nafasi ya kucheza mara kwa mara na hapatti nafasi hiyo klabuni hapo.kalvin PhillipsKalvin Phillips atahakikisha anapambana kwa miezi miwili iliyobaki ndani ya kikosi cha Man City, Lakini mipango yake Januari ikifika akatafute timu ambayo atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara na hofu kubwa kwa kiungo huyo ni kupoteza nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa