Kambwala Ajiunga na Villarreal

Aliyekua beki wa klabu ya Manchester United Willy Kambwala amefanikiwa kujiunga na klabu ya Villarreal ya nchini Hispania baada ya vilabu hivyo viwili kufikia makubaliano.

Willy Kambwala (19) ambaye ameanza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Man United msimu uliomalizika ameuzwa kwa dau la Euro milioni 10 kwenda kwa nyambizi wa njano wa nchini Hispania, Huku kukiwa na kipengelea cha klabu hiyo kuweza kumnunua kwa mara nyingine.kambwalaBeki huyo kinda inaelezwa aligomea mkataba mpya ndani ya Man United kwa kile kilichoelezwa alihitaji muda zaidi wa kucheza, Hivo beki huyo anaamini atapata nafasi ya kucheza zaidi akiwa ndani ya Villarreal tofauti na ambavyo angeendelea kusalia ndani ya kikosi cha Man United.

Kwa kiwango kikubwa maamuzi ya kijana Kambwala yako sahihi kwakua ndani ya Man United kuna ushindani mkubwa wa namba ukizingatia pi anakosa uzoefu mkubwa kulinganisha na mabeki waliopo hapo, Kwani hata msimu uliomalizika alipata nafasi baada ya mabeki wengi wa kati kupata majeraha.kambwalaKlabu ya Man United wao wamekua wajanja kwakua wanaamini bado kijana huyo ana uwezo licha ya kua hakua anapata nafasi ya kutosha ndani yan kikosi chao, Hivo wakamaua kuweka kipengele cha kumnunua tena pale ambapo watakua na uhitaji nae kutokana na ubora ambao atauonesha nchini Hispania.

Acha ujumbe